Mistari ya Biblia Kuhusu Deni
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Deni ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Matajiri huwatawala maskini naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye.
Msidaiwe kitu na mtu yeyote, isipokuwa kupendana, kwa maana yeye ampendaye mwenzake, ameitimiza sheria.
Usiwe mwenye kupana mikono katika rehani, au kuweka dhamana kwa ajili ya madeni. Kama ukikosa njia ya kulipa, kitanda chako kitachukuliwa ukiwa umekilalia.
Waovu hukopa na hawalipi, bali wenye haki hutoa kwa ukarimu.
Kwa kuwa Bwana Mungu wenu atawabariki kama alivyoahidi, nanyi mtawakopesha mataifa mengi lakini hamtakopa kwa yeyote. Mtatawala mataifa mengi lakini hakuna taifa litakalowatawala ninyi.
Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda. Usimwambie jirani yako, “Njoo baadaye, nitakupa kesho”: wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe.
Wakati wote ni wakarimu na hukopesha bila masharti. Watoto wao watabarikiwa.
Yule mwanamke akaenda akamwambia yule mtu wa Mungu, naye mtu wa Mungu akasema, “Nenda ukayauze hayo mafuta ulipe madeni yako. Wewe na wanao mnaweza kuishi kwa kile kinachosalia.”
Yule bwana wa huyo mtumishi akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwacha aende zake.