Mistari ya Biblia Kuhusu Utajiri

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Utajiri ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mithali 11:28

Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka, bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.

02 1 Timotheo 6:17

Waagize wale ambao ni matajiri wa ulimwengu huu waache kujivuna, wala wasiweke tumaini lao katika mali ambayo si ya hakika, bali waweke tumaini lao katika Mungu ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifurahie.

03 Mithali 23:4-5

Usijitaabishe ili kuupata utajiri, uwe na hekima kuonyesha kujizuia. Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka, huwa kama umepata mabawa ghafula, ukaruka na kutoweka angani kama tai.

04 Mhubiri 5:10

Yeyote apendaye fedha kamwe hatosheki na fedha; yeyote apendaye utajiri kamwe hatosheki na kipato chake. Hili nalo pia ni ubatili.

05 Kumbukumbu 8:18

Lakini kumbukeni Bwana Mungu wenu, ndiye ambaye huwapa uwezo wa kupata utajiri, na hivyo kulithibitisha Agano lake, ambalo aliwaapia baba zenu, kama ilivyo leo.

06 Mithali 22:1

Heri kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi, kuheshimiwa ni bora kuliko fedha au dhahabu.

07 Mathayo 6:24

“Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Kwa kuwa atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na Mali.

Mada zinazohusiana