Mistari ya Biblia Kuhusu Jawabu la Upole

Mistari 5 ya Biblia kuhusu Jawabu la Upole ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mithali 15:1

Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira.

02 Mithali 25:15

Kwa njia ya uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa, nao ulimi laini waweza kuvunja mfupa.

03 Mithali 16:24

Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali, ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa.

04 Wakolosai 4:6

Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo na inavyofaa kumjibu kila mtu.

05 Mithali 12:18

Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga, bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.

Mada zinazohusiana