Mistari ya Biblia Kuhusu Chini ya Mbawa Zake

Mistari 14 ya Biblia kuhusu Chini ya Mbawa Zake ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 91:4

Atakufunika kwa manyoya yake, chini ya mbawa zake utapata kimbilio, uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.

02 Zaburi 91:1-2

Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi. Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.”

03 Zaburi 17:8

Nilinde kama mboni ya jicho lako, unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako

04 Zaburi 57:1

Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia mpaka maafa yapite.

05 Mathayo 23:37

“Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!

06 Zaburi 36:7

Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mbawa zako.

07 Zaburi 63:7

Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu, chini ya uvuli wa mbawa zako naimba.

08 Ruthu 2:12

Bwana na akulipe kwa yale uliyoyatenda. Ubarikiwe kwa wingi na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye umekimbilia mabawani mwake.”

09 Zaburi 61:4

Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.

10 Kumbukumbu 32:11

kama tai avurugaye kiota chake, na kurukaruka juu ya makinda yake, ambaye hutanda mabawa yake kuwadaka, na huwachukua kwenye mabawa yake.

11 Luka 13:34

“Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!

12 Malaki 4:2

Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini.

13 Zaburi 91:11

Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako, wakulinde katika njia zako zote.

14 Zaburi 121:5

Bwana anakulinda, Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume,

Mada zinazohusiana