Mistari ya Biblia Kuhusu Unyenyekevu na Utumishi

Yesu, ingawa ni Bwana wa wote, hakuja kutumikiwa, bali kutumika na kutoa nafsi yake. Anatuita tujivike unyenyekevu na kuwahesabu wengine kuwa bora kuliko sisi wenyewe. Aya hizi zinakuongoza katika njia ya chini ambayo Mungu huiinua.

Unyenyekevu — Wafilipi 2:3

Msifanye lolote kwa roho ya kushindana wala kwa tamaa ya sifa tupu. Badala yake, muwe wanyenyekevu, kila mmoja akiwaona wengine kuwa bora kuliko yeye mwenyewe.

Utumishi — Marko 10:45

Kwa kuwa Mwana wa Adamu mwenyewe hakuja ili wengine wamtumikie, bali kuwatumikia na kutoa uhai wake kama gharama ya fidia badala ya wengi.”

Kuwatumikia Wengine — Wagalatia 5:13

Ninyi mliitwa ili muwe huru, ndugu. Ila tu msiruhusu uhuru wenu uwe mwanya kwa asili ya dhambi. Badala yake, kwa upendo, kuweni watumwa ninyi kwa ninyi.

Upole — Wafilipi 4:5

Upole wenu uonekane wazi kwa kila mtu. Bwana yu karibu.

Unyenyekevu wa Moyo — Yakobo 4:10

Jishusheni chini mbele ya Bwana, naye atawainua juu.

Kuwatanguliza Wengine — Wafilipi 2:4

Kila mmoja wenu ajali si mambo yake mwenyewe tu, bali pia mambo ya wengine.

Ukuu katika Ufalme — Mathayo 20:26

Kwenu ni lazima iwe tofauti. Mtu yeyote kati yenu akitaka kuwa mkuu, ni lazima awahudumie wengine.

Kuosha Miguu — Yohana 13:14

Kwa hiyo ikiwa mimi, Bwana na Mwalimu, nimewaosha miguu, basi ninyi pia mna wajibu wa kuoshana miguu.

Mungu Huwainua Wanyenyekevu — 1 Petro 5:6

Basi jinyenyekezeni chini ya mkono wenye nguvu wa Mungu, ili awainue wakati utakapofika.

Kuvikwa Unyenyekevu — 1 Petro 5:5

Hali kadhalika, ninyi mlio vijana, wanyenyekeeni wazee. Na ninyi nyote, mnapohusiana ninyi kwa ninyi, jifungieni unyenyekevu kama vazi, kwa sababu “Mungu anasimama dhidi ya wenye kiburi, lakini wanyenyekevu anawapa neema.”

Nia ya Kristo Ndani Yetu — Wafilipi 2:5

Kati yenu, fikirini kwa namna ambayo Kristo Yesu pia alifikiri.

Upole — Mathayo 5:5

Heri walio wapole: watairithi dunia.