Mistari ya Biblia Kuhusu Kuwatumikia Wengine

Mistari 13 ya Biblia kuhusu Kuwatumikia Wengine ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Wagalatia 5:13

Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo.

02 1 Petro 4:10

Kila mmoja na atumie kipawa chochote alichopewa kuwahudumia wengine, kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu.

03 Mathayo 25:40

“Naye Mfalme atawajibu, ‘Amin nawaambia, kwa jinsi mlivyomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.’

04 Waebrania 6:10

Mungu si mdhalimu: yeye hataisahau kazi yenu na upendo ule mlioonyesha kwa ajili yake katika kuwahudumia watakatifu na hata sasa mnaendelea kuwahudumia.

05 Warumi 12:11

Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana.

06 Wagalatia 6:10

Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio.

07 Marko 10:45

Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”

08 Yohana 13:14

Kwa hiyo, ikiwa mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewanawisha ninyi miguu, pia hamna budi kunawishana miguu ninyi kwa ninyi.

09 Wafilipi 2:4

Kila mmoja wenu asiangalie faida yake mwenyewe tu, bali pia ajishughulishe kwa faida ya wengine.

10 Matendo 20:35

Katika kila jambo nimewaonyesha kwamba kwa njia hii ya kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia wadhaifu, mkikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe jinsi alivyosema, ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea.’ ”

11 1 Wakorintho 12:7

Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote.

12 Mathayo 20:26-27

Isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu, naye anayetaka kuwa wa kwanza miongoni mwenu hana budi kuwa mtumwa wenu:

13 Waefeso 6:7

Tumikeni kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na si wanadamu.

Mada zinazohusiana