Mistari ya Biblia Kuhusu Mungu Huwainua Wanyenyekevu
Mistari 14 ya Biblia kuhusu Mungu Huwainua Wanyenyekevu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake.
Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua.
Kwa maana kila mtu ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa.”
Kwa kuwa yeyote anayejikweza atashushwa, na yeyote anayejinyenyekeza atakwezwa.
Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima.
Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni.
Ingawa Bwana yuko juu, humwangalia mnyonge, bali mwenye kiburi yeye anamjua kutokea mbali.
Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi, bali unyenyekevu hutangulia heshima.
Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu, yeye aliyeinuliwa sana, yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu: “Ninaishi mimi mahali palipoinuka na patakatifu, lakini pia pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na mwenye roho ya unyenyekevu, ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu na kuihuisha mioyo yao waliotubu.
Amewashusha watawala toka kwenye viti vyao vya enzi, lakini amewainua wanyenyekevu.
Unyenyekevu na kumcha Bwana huleta utajiri, heshima na uzima.
Bwana huwahifadhi wanyenyekevu lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini.
Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema: “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
“Nawaambia, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu zaidi ya yule Farisayo. Kwa maana yeyote ajikwezaye atashushwa, na yeyote ajishushaye atakwezwa.”