Mistari ya Biblia Kuhusu Unyenyekevu

Mistari 9 ya Biblia kuhusu Unyenyekevu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Wafilipi 2:3

Msitende jambo lolote kwa nia ya kujitukuza wala kujivuna, bali kwa unyenyekevu kila mtu amhesabu mwingine bora kuliko nafsi yake.

02 Yakobo 4:6

Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema: “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”

03 Mithali 22:4

Unyenyekevu na kumcha Bwana huleta utajiri, heshima na uzima.

04 Mika 6:8

Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu. Bwana anataka nini kwako? Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.

05 Warumi 12:3

Kwa ajili ya neema niliyopewa nawaambia kila mmoja miongoni mwenu, asijidhanie kuwa bora kuliko impasavyo, bali afikiri kwa busara kwa kulingana na kipimo cha imani Mungu aliyompa.

06 1 Petro 5:5

Vivyo hivyo, ninyi mlio vijana watiini wazee. Nanyi nyote imewapasa kujivika unyenyekevu kila mtu kwa mwenzake, kwa kuwa, “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”

07 Mithali 11:2

Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima.

08 Mithali 15:33

Kumcha Bwana humfundisha mtu hekima, nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.

09 Wakolosai 3:12

Kwa hiyo, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.

Mada zinazohusiana