Mistari ya Biblia Kuhusu Utumishi
Mistari 11 ya Biblia kuhusu Utumishi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Kwa kuwa Mwana wa Adamu mwenyewe hakuja ili wengine wamtumikie, bali kuwatumikia na kutoa uhai wake kama gharama ya fidia badala ya wengi.”
Ndivyo ilivyo kwa Mwana wa Adamu. Hakuja ili wengine wamhudumie. Alikuja kuwahudumia, na kutoa uhai wake kuwa fidia kwa ajili ya wengi.”
Nilichowapa ni mfano, ili ninyi pia mfanye kama nilivyowafanyia.
Badala yake, alijifanya mwenyewe kuwa mtupu, akachukua umbo la mtumishi na kushiriki mfano wa wanadamu. Na alipoonekana kwa sura ya nje kama mwanadamu,
Ninyi mliitwa ili muwe huru, ndugu. Ila tu msiruhusu uhuru wenu uwe mwanya kwa asili ya dhambi. Badala yake, kwa upendo, kuweni watumwa ninyi kwa ninyi.
Yeyote aliye mkubwa kuliko wote kati yenu atakuwa ndiye anayewahudumia.
Kila mmoja wenu amepokea karama; itumieni kuhudumiana, kama wasimamizi wazuri wa neema ya Mungu iliyo ya aina nyingi.
Akaketi, akawaita wale Kumi na Wawili, akawaambia, “Mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza lazima awe wa mwisho kuliko wote na mtumishi wa wote.”
Fikirini: ni nani mkubwa zaidi, mgeni aliyeegemea mezani, au yule anayewahudumia chakula? Bila shaka ni yule aliye mezani. Hata hivyo mimi niko hapa kati yenu kama yule anayehudumu.
Ikiwa kumtumikia BWANA kunaonekana vibaya kwenu, basi fanyeni uchaguzi wenu leo. Mtamtumikia nani? Miungu ambayo babu zenu waliitumikia upande wa pili wa Mto, au miungu ya Waamori ambao sasa mnaishi katika nchi yao? Mimi na watu wa nyumbani mwangu tutamtumikia BWANA.”
Lolote mnalofanya, lifanyeni kwa moyo wenu wote, kama kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu, mkijua kwamba mtapokea urithi kutoka kwa Bwana kuwa thawabu yenu. Ni Bwana Kristo mnayemtumikia kama watumwa.