Mistari ya Biblia Kuhusu Ukuu katika Ufalme

Mistari 9 ya Biblia kuhusu Ukuu katika Ufalme ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mathayo 20:26

Isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu,

02 Mathayo 23:11

Yeye aliye mkuu kuliko ninyi nyote miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu.

03 Marko 9:35

Akaketi chini, akawaita wote kumi na wawili, akawaambia: “Kama mtu yeyote akitaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa wa mwisho na mtumishi wa wote.”

04 Luka 22:26

Lakini ninyi msifanane nao. Bali yeye aliye mkuu kuliko wote miongoni mwenu, inampasa kuwa kama yeye aliye mdogo wa wote, naye atawalaye na awe kama yeye ahudumuye.

05 Mathayo 18:4

Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni.

06 Mathayo 18:3

Naye akasema: “Amin, nawaambia, msipookoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni.

07 Luka 9:48

Kisha akawaambia, “Yeyote amkaribishaye mtoto huyu mdogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi, na yeyote atakayenikaribisha mimi, atakuwa amemkaribisha yeye aliyenituma. Kwa maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu, ndiye aliye mkuu kuliko wote.”

08 Mathayo 20:27

naye anayetaka kuwa wa kwanza miongoni mwenu hana budi kuwa mtumwa wenu:

09 Marko 10:43-44

Lakini isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu, na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa mtumwa wa wote.

Mada zinazohusiana