Mistari ya Biblia Kuhusu Kuvikwa Unyenyekevu
Mistari 6 ya Biblia kuhusu Kuvikwa Unyenyekevu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Hali kadhalika, ninyi mlio vijana, wanyenyekeeni wazee. Na ninyi nyote, mnapohusiana ninyi kwa ninyi, jifungieni unyenyekevu kama vazi, kwa sababu “Mungu anasimama dhidi ya wenye kiburi, lakini wanyenyekevu anawapa neema.”
Ninyi ni watu wa Mungu aliowachagua, watakatifu, na mnaopendwa na yeye. Kwa hiyo vaeni, kama mavazi, moyo wenye huruma, fadhili, unyenyekevu, upole na subira.
Basi jinyenyekezeni chini ya mkono wenye nguvu wa Mungu, ili awainue wakati utakapofika.
Msifanye lolote kwa roho ya kushindana wala kwa tamaa ya sifa tupu. Badala yake, muwe wanyenyekevu, kila mmoja akiwaona wengine kuwa bora kuliko yeye mwenyewe.
Kiburi kinapofika, fedheha hufuata nyuma yake, bali wanyenyekevu wana hekima.
Lakini neema anayoitoa ni kubwa zaidi. Ndiyo maana inasema, “Mungu anasimama dhidi ya wenye kiburi, lakini wanyenyekevu anawapa neema.”