Mistari ya Biblia Kuhusu Neno Ladumu Milele
Mistari 10 ya Biblia kuhusu Neno Ladumu Milele ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Majani hunyauka na maua huanguka, lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”
Maana, “Wanadamu wote ni kama majani, nao utukufu wao ni kama maua ya kondeni; majani hunyauka na maua huanguka, lakini neno la Bwana ladumu milele.” Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.
Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Ee Bwana, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni.
Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako kwamba umezithibitisha ili zidumu milele.
Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
Kwa maana Bwana ni mwema na upendo wake wadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.
“Kwa habari yangu mimi, hili ndilo agano langu nao,” asema Bwana. “Roho wangu, aliye juu yenu, na maneno yangu ambayo nimeyaweka katika vinywa vyenu, havitaondoka vinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwa watoto wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao, kuanzia sasa na hata milele,” asema Bwana.
Maneno ya Bwana ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba. Ee Bwana, utatuweka salama na kutulinda na kizazi hiki milele.