Mistari ya Biblia Kuhusu Mtu Hataishi kwa Mkate Peke Yake

Mistari 11 ya Biblia kuhusu Mtu Hataishi kwa Mkate Peke Yake ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 11 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Mathayo 4:4 Mstari mkuu

Lakini Yesu alijibu, “Maandiko yanasema, ‘Hakuna mtu anayeishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.’”

Alikushusha chini na kukuacha uone njaa, kisha akakulisha mana, chakula ambacho wewe wala mababu zako hamkuwahi kukijua. Alifanya hivyo ili akufundishe kwamba watu hawaishi kwa mkate peke yake, bali wanaishi kwa kila kitu kinachotoka kinywani mwa BWANA.

03 Luka 4:4

Yesu alimjibu, “Maandiko yanasema, ‘Binadamu haishi kwa mkate peke yake.’”

04 Yohana 6:35

Yesu akawaambia, “Mimi ni mkate wa uzima. Wanaokuja kwangu hawatakuwa na njaa kamwe, na wanaoniamini hawatakuwa na kiu wakati wowote.

05 Yohana 6:51

Mimi ni mkate ulio hai, ulioshuka kutoka mbinguni. Mtu yeyote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate nitakaoutoa ni mwili wangu, nami nautoa ili ulimwengu upate uzima.”

06 Yohana 6:63

Roho ndiye anayetoa uzima; mwili haufai kitu chochote. Maneno niliyowaambia ni roho, nayo ni uzima.

07 Yohana 6:68

Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tungeenda kwa nani? Una maneno yanayoleta uzima wa milele.

08 1 Petro 2:2

Kama vichanga vilivyozaliwa karibuni, tamanini sana maziwa safi ya neno la Mungu, ili kwa hayo mkue mpaka mfikie wokovu,

09 Yohana 4:34

Yesu akawaambia, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya yule aliyenituma, na kuikamilisha kazi yake.”

10 Mithali 9:5

“Njooni, mle chakula changu na kuonja divai niliyoichanganya.

11 Zaburi 119:103

Jinsi kauli zako zinavyonitamu, tamu kuliko asali ulimini mwangu!

Mada zinazohusiana