Mistari ya Biblia Kuhusu Kuliweka Neno Moyoni

Mistari 6 ya Biblia kuhusu Kuliweka Neno Moyoni ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 119:11

Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.

02 Kumbukumbu 6:6-7

Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.

03 Wakolosai 3:16

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu.

04 Zaburi 119:9

Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.

05 Mithali 7:1-3

Mwanangu, shika maneno yangu na kuzihifadhi amri zangu ndani yako. Shika amri zangu nawe utaishi; linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. Yafunge katika vidole vyako; yaandike katika kibao cha moyo wako.

06 Kumbukumbu 11:18

Yawekeni haya maneno yangu katika mioyo yenu na akili zenu, yafungeni kama alama juu ya mikono yenu na kwenye paji za nyuso zenu.

Mada zinazohusiana