Mistari ya Biblia Kuhusu Taa ya Miguu Yangu
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Taa ya Miguu Yangu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.
Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru, kunampa mjinga ufahamu.
Kwa maana amri hizi ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,
Nasi tunalo pia neno la hakika zaidi la unabii, ambalo mtafanya vyema mkiliangalia kwa bidii, kama vile nuru inavyongʼaa gizani, hadi kupambazuka na nyota ya asubuhi izuke mioyoni mwenu.
Kisha Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu yeyote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”
Maagizo ya Bwana ni kamili, nayo hufurahisha moyo. Amri za Bwana huangaza, zatia nuru machoni.
Tuma hima nuru yako na kweli yako na viniongoze; vinilete mpaka mlima wako mtakatifu, mpaka mahali unapoishi.
Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko, ambayo hungʼaa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu.
Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.