Mistari ya Biblia Kuhusu Kulisimamia Neno
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Kulisimamia Neno ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Majani hunyauka na maua huanguka, lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”
lakini neno la Bwana ladumu milele.” Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.
“Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba. Lakini haikuanguka; kwa sababu msingi wake ulikuwa kwenye mwamba.
Ee Bwana, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni.
Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
Maneno yako yote ni kweli, sheria zako zote za haki ni za milele.
Kama aliwaita ‘miungu,’ wale ambao neno la Mungu liliwafikia, nayo Maandiko hayawezi kutanguka,
ndivyo lilivyo neno langu lile litokalo kinywani mwangu: Halitanirudia tupu, bali litatimiliza lile nililokusudia na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma.