Mistari ya Biblia Kuhusu Tamu Kuliko Asali

Mistari 15 ya Biblia kuhusu Tamu Kuliko Asali ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 119:103

Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu!

02 Zaburi 19:10

Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega.

03 Zaburi 119:97

Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa.

04 Yeremia 15:16

Maneno yako yalipokuja, niliyala; yakawa shangwe yangu na furaha ya moyo wangu, kwa kuwa nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.

05 Ezekieli 3:3

Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, kula ukurasa huu wa kitabu ninaokupa ujaze tumbo lako.” Kwa hiyo nikaula, ulikuwa mtamu kama asali kinywani mwangu.

06 Zaburi 119:72

Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.

07 Zaburi 119:127

Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu, naam, zaidi ya dhahabu safi,

08 Zaburi 119:111

Sheria zako ni urithi wangu milele, naam ni furaha ya moyo wangu.

09 Mithali 24:13-14

Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri; asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja. Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako, kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo, nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali.

10 Zaburi 19:9-10

Kumcha Bwana ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za Bwana ni za hakika, nazo zina haki. Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega.

11 Zaburi 119:162

Nafurahia ahadi zako kama mtu aliyepata mateka mengi.

12 Ayubu 23:12

Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake; nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku.

13 Zaburi 119:131

Nimefungua kinywa changu na kuhema, nikitamani amri zako.

14 Zaburi 119:14

Ninafurahia kufuata sheria zako kama mtu afurahiaye mali nyingi.

15 Mithali 16:24

Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali, ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa.

Mada zinazohusiana