Mistari ya Biblia Kuhusu Kulitafakari Neno
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Kulitafakari Neno ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Usiache Kitabu hiki cha Sheria kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi.
Bali huifurahia sheria ya Bwana, naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana. Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa.
Ninatafakari maagizo yako na kuziangalia njia zako.
Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa.
Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo.
Sikufumba macho yangu usiku kucha, ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako.
Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.
Nakumbuka siku za zamani; natafakari juu ya kazi zako zote, naangalia juu ya kazi ambazo mikono yako imezifanya.
Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu.