Mistari ya Biblia Kuhusu Nguvu ya Ulimi

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Nguvu ya Ulimi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mithali 18:21

Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao waupendao watakula matunda yake.

02 Yakobo 3:5-6

Vivyo hivyo ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili, lakini hujivuna majivuno makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa! Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa jehanamu.

03 Mithali 12:18

Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga, bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.

04 Mithali 15:4

Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima, bali ulimi udanganyao huponda roho.

05 Mathayo 12:36-37

Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu kuhusu kila neno lisilo maana walilonena. Kwa maana kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.”

06 Yakobo 3:8

lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

07 Mithali 21:23

Yeye alindaye kinywa chake na ulimi wake hujilinda na maafa.

Mada zinazohusiana