Mistari ya Biblia Kuhusu Uzuri wa Utakatifu
Mistari 11 ya Biblia kuhusu Uzuri wa Utakatifu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Inameni mbele za BWANA katika fahari takatifu; tetemekeni mbele yake, dunia yote.
Nimemwomba BWANA jambo moja, nalo ndilo ninalolitafuta: kuishi katika nyumba ya BWANA maisha yangu yote, kuutazama upendezo wa BWANA na kumtafuta yeye katika hekalu lake.
Mpeni BWANA utukufu unaostahili jina lake; leteni zawadi mkaje mbele zake; inameni mbele za BWANA katika fahari takatifu.
Kirini utukufu unaolistahili jina la BWANA; inameni mbele za BWANA katika fahari takatifu.
Bwana Mungu wetu na atuonyeshe wema wake. Uipe kazi ya mikono yetu thamani ya kudumu; naam, uipe kazi ya mikono yetu thamani ya kudumu.
Baada ya kushauriana na watu, aliweka waimbaji wamwimbie BWANA na kumsifu katika uzuri wa utakatifu walipotangulia mbele ya jeshi, wakisema, “Mshukuruni BWANA, kwa maana upendo wake usiokoma unadumu milele.”
Fahari na enzi vimesimama mbele yake; nguvu na uzuri vimejaa mahali pake patakatifu.
Nitaitafakari enzi yako, utukufu wake na fahari yake, na habari za maajabu yako.
Mungu ameng’aa kwa nguvu kutoka Sayuni, mji wa uzuri usio na kasoro.
Umshonee ndugu yako Haruni mavazi matakatifu, ili yampe utukufu na uzuri.
Watu wako wanajitoa kwa hiari siku unapotoka kwa nguvu, katika fahari na utakatifu. Kutoka tumbo la alfajiri ujana wako unakujia ukiwa safi kama umande.