Mistari ya Biblia Kuhusu Msifuni Mahali Palipo Juu
Mistari 13 ya Biblia kuhusu Msifuni Mahali Palipo Juu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Msifuni Bwana. Msifuni Bwana kutoka mbinguni, msifuni juu vileleni.
Msifuni, enyi malaika wake wote, msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni. Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo.
Wote na walisifu jina la Bwana, kwa maana jina lake pekee limetukuka, utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu.
Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, anga zahubiri kazi ya mikono yake.
Msifuni Bwana. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu.
Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana. Msifuni Bwana!
Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako, uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu.
Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni Bwana Mwenye Nguvu Zote; dunia yote imejaa utukufu wake.”
Kila mmoja wa hawa viumbe wanne wenye uhai alikuwa na mabawa sita, na kujawa na macho pande zote hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawaachi kusema: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.”
Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;
Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana, na ninyi maji juu ya anga.
Wewe peke yako ndiwe Bwana. Uliziumba mbingu, hata mbingu za mbingu na jeshi lote la mbinguni, dunia na vyote vilivyo ndani yake, na pia bahari na vyote vilivyomo ndani yake. Huvipa vitu vyote uhai, nalo jeshi la mbinguni linakuabudu wewe.
Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, ninyi mlio mashujaa mnaozitii amri zake, ninyi mnaotii neno lake. Mhimidini Bwana, ninyi jeshi lake lote la mbinguni, ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake.