Mistari ya Biblia Kuhusu Ibada katika Roho na Kweli

Mistari 12 ya Biblia kuhusu Ibada katika Roho na Kweli ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Yohana 4:23

Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta.

02 Yohana 4:24

Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

03 Wafilipi 3:3

Kwa maana sisi ndio tulio tohara, sisi tumwabuduo Mungu katika Roho, tunaona fahari katika Kristo Yesu, ambao hatuweki tumaini letu katika mwili,

04 Warumi 12:1

Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana.

05 Zaburi 145:18

Bwana yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.

06 Waebrania 10:22

sisi na tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu kwa imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa damu ya Kristo na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya nayo miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi.

07 Zaburi 51:17

Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau.

08 1 Samweli 16:7

Lakini Bwana akamwambia Samweli, “Usitazame sura yake wala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa. Bwana hatazami katika vile vitu mwanadamu avitazamavyo. Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini Bwana hutazama moyoni.”

09 Mathayo 15:8-9

“ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. Huniabudu bure; nayo mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu tu.’ ”

10 Yohana 4:21

Yesu akamjibu, “Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu.

11 Matendo 17:24-25

“Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, yeye ndiye Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu. Wala hatumikiwi na mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji chochote, kwa sababu yeye mwenyewe ndiye awapaye watu wote uhai na pumzi na vitu vyote.

12 Zaburi 24:3-4

Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana? Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake? Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo.

Mada zinazohusiana