Mistari ya Biblia Kuhusu Kumwimbia Mungu
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Kumwimbia Mungu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya; mwimbieni Bwana dunia yote.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu; kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu umemfanyia wokovu.
Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu,
Mwabuduni Bwana kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu.
Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu.
Mwimbieni Bwana kwa shukrani, mpigieni Mungu wetu kinubi.
Mwimbieni wimbo mpya; pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe.
Nitamwimbia Bwana maisha yangu yote; nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi.