Mistari ya Biblia Kuhusu Kuabudu
Mistari 12 ya Biblia kuhusu Kuabudu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Njooni, tusujudu mpaka chini na kuinama; tupige magoti mbele za BWANA, yeye aliyetuumba.
Mwinueni juu BWANA Mungu wetu, msujudu mbele ya kiti chake cha miguu. Yeye ni mtakatifu!
“Bwana wetu na Mungu wetu, wewe unastahili kupokea utukufu, heshima na uweza, kwa sababu wewe uliviumba vitu vyote: kwa kuwa ulipenda, vilikuwepo na viliumbwa.”
Kirini utukufu unaolistahili jina la BWANA; inameni mbele za BWANA katika fahari takatifu.
Inameni mbele za BWANA katika fahari takatifu; tetemekeni mbele yake, dunia yote.
Ee BWANA, Bwana wetu, jina lako lina utukufu ulioje duniani kote! Fahari yako inafika juu kuliko mbingu.
Walisema kwa sauti kubwa, “Mwanakondoo aliyechinjwa anastahili kupokea uweza, utajiri, hekima, nguvu, heshima, utukufu na sifa!”
Kisha nilisikia kila kiumbe mbinguni, duniani, chini ya dunia na baharini, na vyote vilivyomo, vikisema: “Kwa yeye aliyeketi juu ya kiti cha enzi na kwa Mwanakondoo kuwe na sifa na heshima na utukufu na uweza milele na milele!”
BWANA ni mkuu, anastahili sifa za juu kabisa, na hakuna awezaye kuchunguza kina cha ukuu wake.
Upendo wako usiokoma una thamani kuliko uhai, kwa hiyo midomo yangu itaimba sifa zako.
Mpeni BWANA utukufu unaostahili jina lake; leteni zawadi mkaje mbele zake; inameni mbele za BWANA katika fahari takatifu.
Kuanzia mahali jua linapochomoza mpaka linapotua, jina la BWANA linastahili kusifiwa.