Mistari ya Biblia Kuhusu Ibada
Mistari 10 ya Biblia kuhusu Ibada ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Mungu ni roho, na yeyote anayemwabudu lazima afanye hivyo katika roho na kweli.”
Kirini utukufu unaolistahili jina la BWANA; inameni mbele za BWANA katika fahari takatifu.
Basi ndugu, nawasihi kwa rehema za Mungu: mtoe miili yenu kwa Mungu kama dhabihu hai, takatifu na inayompendeza. Hiyo ndiyo ibada yenu ya busara.
“Bwana wetu na Mungu wetu, wewe unastahili kupokea utukufu, heshima na uweza, kwa sababu wewe uliviumba vitu vyote: kwa kuwa ulipenda, vilikuwepo na viliumbwa.”
Mtumikieni BWANA huku mkifurahi; njooni mbele yake kwa vigelegele vya furaha.
Njooni, tusujudu mpaka chini na kuinama; tupige magoti mbele za BWANA, yeye aliyetuumba.
Inameni mbele za BWANA katika fahari takatifu; tetemekeni mbele yake, dunia yote.
Basi, kwa kuwa tunapewa ufalme ambao hakuna kitu kinachoweza kuutikisa, tushike shukrani, na kupitia hiyo tumtumikie Mungu katika ibada kwa namna inayompendeza, kwa uchaji na hofu kuu.
Usimsujudie mungu mwingine yeyote. BWANA anaitwa Mwenye Wivu; yeye ni Mungu mwenye wivu.
Mwinueni juu BWANA Mungu wetu, msujudu mbele ya kiti chake cha miguu. Yeye ni mtakatifu!