Mistari ya Biblia Kuhusu Mhimidi Bwana

Mistari 9 ya Biblia kuhusu Mhimidi Bwana ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 103:1

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Vyote vilivyomo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu.

02 Zaburi 103:2

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, wala usisahau wema wake wote,

03 Zaburi 34:1

Nitamtukuza Bwana nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.

04 Zaburi 104:1

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Ee Bwana Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi.

05 Zaburi 145:1-2

Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele. Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele.

06 Zaburi 103:22

Mhimidini Bwana, kazi zake zote kila mahali katika milki yake. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.

07 Zaburi 16:7

Nitamsifu Bwana ambaye hunishauri, hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha.

08 Zaburi 115:18

bali ni sisi tunaomtukuza Bwana, sasa na hata milele. Msifuni Bwana.

09 Zaburi 134:1

Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana.

Mada zinazohusiana