Mistari ya Biblia Kuhusu Sifa
Mistari 8 ya Biblia kuhusu Sifa ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
01 Zaburi 150:6
Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana. Msifuni Bwana!
02 Zaburi 34:1
Nitamtukuza Bwana nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.
03 Zaburi 145:3
Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki.
04 Zaburi 9:1
Ee Bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.
Basi kwa njia ya Yesu, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani matunda ya midomo inayolikiri Jina lake.
06 Zaburi 147:1
Msifuni Bwana. Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa, jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye!
07 Zaburi 103:1
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Vyote vilivyomo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu.
08 Zaburi 71:8
Kinywa changu kimejazwa sifa zako, nikitangaza utukufu wako mchana kutwa.