Mistari ya Biblia Kuhusu Enenda kwa Hekima
Mistari 10 ya Biblia kuhusu Enenda kwa Hekima ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Ishini kwa hekima mnapohusiana na watu walio nje ya kanisa, mkitumia vizuri kila nafasi.
Kwa hiyo jihadharini sana jinsi mnavyoishi, si kama watu wasio na busara, bali kama watu wenye busara. Tumieni vizuri kila nafasi, kwa sababu siku ni mbaya.
Ikiwa mmoja wenu anakosa hekima, amwombe Mungu, anayewapa watu wote kwa mkono wazi bila kuwasuta, naye atapewa.
Hekima huanzia hapa: pata hekima. Tumia vyote ulivyo navyo, ikibidi, ili upate ufahamu.
Ndiyo sababu, tangu siku tuliposikia habari zenu, hatujaacha kusali kwa ajili yenu. Tunamwomba Mungu awajaze ujuzi wa mapenzi yake, pamoja na hekima yote na ufahamu unaotoka kwa Roho, ili mpate kuishi maisha yanayomstahili Bwana na kumpendeza katika kila jambo, mkizaa matunda katika kila aina ya kazi njema na kukua katika kumjua Mungu.
Mwamini BWANA kwa moyo wako mzima, wala usijiegemeze kwenye busara yako mwenyewe. Mkumbuke yeye katika kila unalofanya, naye atakutengenezea njia iliyonyooka mbele yako.
Hekima huanza kwa kumcha BWANA, na kumjua Mtakatifu ndio ufahamu.
Lakini hekima inayotoka juu, kwanza kabisa, ni safi. Tena huleta amani; ni ya kiungwana na iko tayari kukubali hoja za wengine; imejaa rehema na matunda mazuri; haipendelei mtu, wala haijifanyi.
Basi, utufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri, ili mioyo yetu ipate hekima.
Kwa maana ni BWANA atoaye hekima; maarifa na ufahamu hutoka kinywani mwake.