Mistari ya Biblia Kuhusu Ufahamu
Mistari 14 ya Biblia kuhusu Ufahamu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Heri mtu yule aonaye hekima, mtu yule apataye ufahamu,
Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima. Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.
kutega sikio lako kwenye hekima na kuweka moyo wako katika ufahamu, na kama ukiita busara na kuita kwa sauti ufahamu,
Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu, kuchagua ufahamu kuliko fedha!
Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru, kunampa mjinga ufahamu.
Naye Mungu akamwambia mwanadamu, ‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima, nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”
“Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.
Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu bali haijulikani miongoni mwa wapumbavu.
Ndugu zangu, msiwe kama watoto katika kufikiri kwenu, afadhali kuhusu uovu mwe kama watoto wachanga, lakini katika kufikiri kwenu, mwe watu wazima.
Mpumbavu hafurahii ufahamu, bali hufurahia kutangaza maoni yake mwenyewe.
Kwa sababu hii, tangu siku ile tuliposikia habari zenu, hatujakoma kuomba kwa ajili yenu na kumsihi Mungu awajaze ninyi maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote ya kiroho na ufahamu.
Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe, yeye ahifadhiye ufahamu hustawi.