Mistari ya Biblia Kuhusu Hekima Itokayo Juu

Mistari 11 ya Biblia kuhusu Hekima Itokayo Juu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Yakobo 3:17

Lakini hekima itokayo mbinguni kwanza ni safi, kisha inapenda amani, tena ni ya upole, iliyo tayari kusikiliza wengine kwa unyenyekevu, iliyojaa huruma na matunda mema, isiyopendelea mtu, tena isiyokuwa na unafiki.

02 Yakobo 1:5

Kama mtu yeyote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa.

03 1 Wakorintho 1:25

Kwa maana upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu.

04 Mithali 2:6

Kwa maana Bwana hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.

05 Wakolosai 1:9

Kwa sababu hii, tangu siku ile tuliposikia habari zenu, hatujakoma kuomba kwa ajili yenu na kumsihi Mungu awajaze ninyi maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote ya kiroho na ufahamu.

06 1 Wakorintho 1:30

Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu, yaani haki, na utakatifu na ukombozi.

07 Danieli 2:20-21

na akasema: “Lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; hekima na uweza ni vyake. Yeye hubadili nyakati na majira; huwaweka wafalme na kuwaondoa. Huwapa hekima wenye hekima, na maarifa wenye ufahamu.

08 Waefeso 1:17

Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi.

09 Mithali 8:22-23

“ Bwana aliniumba mwanzoni mwa kazi yake, kabla ya matendo yake ya zamani; niliteuliwa tangu milele, tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa.

10 1 Wakorintho 2:6-7

Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika. Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu.

11 Ayubu 28:23-28

Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa, kwa maana yeye huitazama miisho ya dunia na huona kila kitu chini ya mbingu. Alipofanyiza nguvu za upepo na kuyapima maji, alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua na njia kwa ajili ya umeme wa radi, ndipo alipoitazama hekima na kuikadiria thamani yake, akaithibitisha na kuihakikisha. Naye Mungu akamwambia mwanadamu, ‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima, nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”

Mada zinazohusiana