Mistari ya Biblia Kuhusu Maarifa

Mistari 8 ya Biblia kuhusu Maarifa ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mithali 1:7

Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.

02 Hosea 4:6

watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, “Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeacha kuijali sheria ya Mungu wako mimi nami sitawajali watoto wako.

03 Mithali 2:5

ndipo utakapoelewa kumcha Bwana na kupata maarifa ya Mungu.

04 2 Petro 3:18

Bali kueni katika neema na katika kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na milele! Amen.

05 Wafilipi 1:9

Haya ndiyo maombi yangu: kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote,

06 Mithali 9:10

“Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.

07 Wakolosai 2:3

ambaye ndani yake kumefichwa hazina zote za hekima na maarifa.

08 Mithali 18:15

Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa, masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa.

Mada zinazohusiana