Mistari ya Biblia Kuhusu Mwongozo
Mistari 10 ya Biblia kuhusu Mwongozo ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Nitakupa ufahamu na kukuonyesha njia unayopaswa kuifuata; nitakushauri na kukuangalia kwa jicho langu.
Mwamini BWANA kwa moyo wako mzima, wala usijiegemeze kwenye busara yako mwenyewe. Mkumbuke yeye katika kila unalofanya, naye atakutengenezea njia iliyonyooka mbele yako.
Lakini yeye, Roho wa kweli, atakapokuja, atawaongoza katika kweli yote. Atakayoyasema hayatatoka kwake mwenyewe; atasema yale anayoyasikia, na atawajulisha mambo yatakayokuja.
Anawaelekeza wanyonge katika yaliyo ya haki, na wanyonge anawafundisha njia yake.
kwamba huyu ndiye Mungu, Mungu wetu milele na daima; yeye atakuwa kiongozi wetu mpaka tufe.
Unaniongoza kwa mashauri yako ya hekima, na mwishowe wewe utanichukua katika utukufu.
Uniongoze kwa uaminifu wako na unifundishe, kwa kuwa wewe ndiwe Mungu anayeniokoa; ni wewe ninayekungoja siku nzima.
Watu hupanga njia zao mioyoni mwao, bali ni BWANA anayeziongoza hatua zao.
Unifundishe kutenda yanayokupendeza, kwa kuwa wewe ni Mungu wangu. Roho wako, aliye mwema, aniongoze katika ardhi tambarare.
Kwa upendo wako usiokoma uliwaongoza watu uliowakomboa; kwa nguvu zako uliwafikisha kwenye makao yako matakatifu.