Mistari ya Biblia Kuhusu Dhabihu ya Sifa

Mistari 8 ya Biblia kuhusu Dhabihu ya Sifa ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 8 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Waebrania 13:15 Mstari mkuu

Kwa hiyo kupitia yeye tumtolee Mungu dhabihu ya sifa wakati wote: tunda la midomo inayotoa shukrani kwa jina lake.

02 Zaburi 50:23

Anayetoa shukrani kama dhabihu ananipa heshima, na anayetembea katika njia iliyonyooka nitamwonyesha jinsi Mungu anavyookoa.”

03 Waebrania 13:16

Tena msisahau kuwa wema na kugawana mlicho nacho ninyi kwa ninyi: Mungu hufurahia dhabihu za aina hiyo.

04 Zaburi 116:17

Nitakuletea sadaka ya shukrani na kumwita BWANA kwa jina lake.

05 Zaburi 27:6

Basi sasa nitakiinua kichwa changu juu ya adui wanaonizunguka; katika hema lake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe, nami nitamwimbia BWANA na kumpigia muziki.

06 Zaburi 107:22

Na walete sadaka za shukrani, na kwa kelele za furaha wasimulie aliyoyatenda.

07 Zaburi 54:6

Nitakutolea wewe dhabihu kwa hiari yangu mwenyewe; Ee BWANA, nitakushukuru na kuliheshimu jina lako, kwa maana ni jema.

08 Zaburi 141:2

Maombi yangu na yasimame mbele yako kama uvumba, mikono yangu iliyoinuliwa kama sadaka ya jioni.

Mada zinazohusiana