Mistari ya Biblia Kuhusu Mungu Aonaye
Mistari 13 ya Biblia kuhusu Mungu Aonaye ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Hagari akampa Bwana aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.”
Macho ya Bwana yako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema.
Ee Bwana, umenichunguza na kunijua. Unajua ninapoketi na ninapoinuka; unatambua mawazo yangu tokea mbali.
Wala hakuna kiumbe chochote kilichofichika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye kwake ni lazima tutatoa hesabu.
Kwa kuwa macho ya Bwana hukimbiakimbia duniani kote ili kujionyesha mwenye nguvu kwa ajili ya wale ambao mioyo yao inamtegemea kwa ukamilifu. Umefanya jambo la upumbavu na kuanzia sasa na kuendelea utakuwa na vita.”
Kutoka mbinguni Bwana hutazama chini na kuwaona wanadamu wote; kutoka maskani mwake huwaangalia wote wakaao duniani: yeye ambaye huumba mioyo yao wote, ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda.
Je, mtu yeyote aweza kujificha mahali pa siri ili nisiweze kumwona?” Bwana asema. “Je, mimi sikuijaza mbingu na nchi?” Bwana asema.
Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; nikifanya vilindi kuwa kitanda changu, wewe uko huko. Kama nikipanda juu ya mbawa za mapambazuko, kama nikikaa pande za mbali za bahari, hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti.
“Macho yake yanazitazama njia za wanadamu; anaona kila hatua yao.
Bwana yuko ndani ya Hekalu lake takatifu; Bwana yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni. Huwaangalia wana wa watu, macho yake yanawajaribu.
Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana, naye huyapima mapito yake yote.
Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia, hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi.
Mnajua kwamba shomoro watano huuzwa kwa senti mbili? Lakini Mungu hamsahau hata mmoja wao. Naam, hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. Hivyo msiogope, kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.