Mistari ya Biblia Kuhusu Mwenyezi

Mistari 11 ya Biblia kuhusu Mwenyezi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Ufunuo 1:8

“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”

02 Mwanzo 17:1

Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, Bwana akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi; enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu.

03 Ufunuo 4:8

Kila mmoja wa hawa viumbe wanne wenye uhai alikuwa na mabawa sita, na kujawa na macho pande zote hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawaachi kusema: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.”

04 Zaburi 91:1

Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.

05 Ayubu 42:2

“Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote, wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.

06 Yeremia 32:17

“Ee Bwana Mwenyezi, umeumba mbingu na nchi kwa uwezo wako mkuu na kwa mkono ulionyooshwa. Hakuna jambo lililo gumu usiloliweza.

07 Mwanzo 1:1

Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.

08 Isaya 40:28

Je wewe, hufahamu? Je wewe, hujasikia? Bwana ni Mungu wa milele, Muumba wa miisho ya dunia. Hatachoka wala kulegea, wala hakuna hata mmoja awezaye kuupima ufahamu wake.

09 Mathayo 19:26

Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini mambo yote yanawezekana kwa Mungu.”

10 Zaburi 147:5

Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, ufahamu wake hauna kikomo.

11 Ufunuo 15:3

Nao wakaimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema: “ Bwana Mungu Mwenyezi, matendo yako ni makuu na ya ajabu. Njia zako wewe ni za haki na za kweli, Mfalme wa nyakati zote!

Mada zinazohusiana