Mistari ya Biblia Kuhusu Yehova Yire (Bwana Hutoa)
Mistari 11 ya Biblia kuhusu Yehova Yire (Bwana Hutoa) ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire. Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa Bwana itapatikana.”
Naye Mungu wangu atawajaza ninyi na kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Kristo Yesu.
Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.
Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Abrahamu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.
Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema.
Mcheni Bwana enyi watakatifu wake, kwa maana wale wamchao hawapungukiwi na chochote. Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wamtafutao Bwana hawatakosa kitu chochote kilicho chema.
Bali utafuteni Ufalme wa Mungu, na haya yote atawapa pia.
Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja naye?
Huwapa chakula wale wanaomcha, hulikumbuka agano lake milele.