Mistari ya Biblia Kuhusu Mwamba

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Mwamba ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 18:2

Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu.

02 Kumbukumbu 32:4

Yeye ni Mwamba, kazi zake ni kamilifu, njia zake zote ni haki. Mungu mwaminifu ambaye hakosei, yeye ni mnyofu na mwenye haki.

03 Zaburi 62:2

Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe.

04 1 Samweli 2:2

“Hakuna yeyote aliye mtakatifu kama Bwana, hakuna mwingine zaidi yako; hakuna Mwamba kama Mungu wetu.

05 Zaburi 18:31

Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu?

06 2 Samweli 22:2-3

Akasema: “ Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba wangu, ambaye kwake ninakimbilia, ngao yangu na pembe ya wokovu wangu. Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu na mwokozi wangu, huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri.

07 Isaya 26:4

Mtumaini Bwana milele, kwa kuwa Bwana, Bwana, ni Mwamba wa milele.

Mada zinazohusiana