Mistari ya Biblia Kuhusu Wasemee Wasio na Sauti
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Wasemee Wasio na Sauti ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
“Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea, kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa. Sema na uamue kwa haki, tetea haki za maskini na wahitaji.”
jifunzeni kutenda mema! Tafuteni haki, watieni moyo walioonewa. Teteeni shauri la yatima, wateteeni wajane.
Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa. Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.
Hili ndilo Bwana asemalo: Tenda haki na adili. Mwokoe mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane, wala usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa.
Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo; wazuie wote wanaojikokota kuelekea machinjoni. Kama mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,” je, yule apimaye mioyo halitambui hili? Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili? Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda?
kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada, naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia.
Heri mtu yule anayemjali mnyonge, Bwana atamwokoa wakati wa shida.
Kwa kuwa kama utakaa kimya wakati huu, msaada na ukombozi kwa Wayahudi utatoka mahali pengine, lakini wewe na jamaa ya baba yako mtaangamia. Nani ajuaye kwamba hukuja kwenye nafasi ya mamlaka kwa ajili ya wakati kama huu?”
Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishughulishi na hilo.