Mistari ya Biblia Kuhusu Upendo Haukomi

Mistari 8 ya Biblia kuhusu Upendo Haukomi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 8 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 1 Wakorintho 13:8 Mstari mkuu

Upendo haufikii mwisho kamwe. Lakini unabii utaondolewa; lugha zitanyamaza; maarifa yataondolewa.

02 1 Wakorintho 13:13

Basi kama mambo yalivyo, vitu vitatu vinadumu: imani, tumaini na upendo. Na kati ya vitu hivi vitatu, kilicho kikuu kabisa ni upendo.

03 Warumi 8:38-39

Kwa maana nina hakika kabisa kwamba si kifo wala uzima, si malaika wala watawala, si mambo yaliyopo sasa wala yale yatakayokuja, si nguvu zozote, si vilivyo juu sana wala vilivyo chini kabisa, wala kitu kingine chochote kilichoumbwa: hakuna kitakachoweza kutukatilia mbali na upendo wa Mungu, ambao ni wetu katika Kristo Yesu Bwana wetu.

04 1 Wakorintho 13:7

Hakuna jambo ambalo upendo hauwezi kulibeba, hakuna wakati unapoacha kuamini au kutumaini, hakuna jambo usiloweza kulistahimili.

05 Warumi 8:35

Ni nani anayeweza kutung’oa kutoka katika upendo wa Kristo? Je, ni taabu, au dhiki, au kuteswa? Je, ni njaa, au kukosa mavazi, au hatari, au upanga?

06 1 Yohana 4:18

Upendo hauna nafasi ya hofu; badala yake, upendo kamili huifukuza hofu, kwa sababu hofu inahusiana na adhabu, na yeyote anayeogopa hajafikia lengo la upendo.

07 Zaburi 136:1

Mshukuruni BWANA, kwa maana yeye ni mwema; upendo wake usiokoma unadumu milele.

08 Yohana 13:1

Ilikuwa kabla kidogo ya sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua kwamba saa yake ilikuwa imefika, saa ya kutoka katika ulimwengu huu kwenda kwa Baba. Alikuwa amewapenda walio wake waliokuwa ulimwenguni, naye aliwapenda mpaka mwisho.

Mada zinazohusiana