Mistari ya Biblia Kuhusu Ukarimu wa Moyo

Mistari 6 ya Biblia kuhusu Ukarimu wa Moyo ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 6 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Waefeso 4:32 Mstari mkuu

Kuweni wema kwa kila mmoja wenu na wenye huruma nyingi. Sameheaneni kwa moyo mkunjufu, kama vile Mungu alivyowasamehe ninyi katika Kristo.

02 Wakolosai 3:12

Ninyi ni watu wa Mungu aliowachagua, watakatifu, na mnaopendwa na yeye. Kwa hiyo vaeni, kama mavazi, moyo wenye huruma, fadhili, unyenyekevu, upole na subira.

03 Wagalatia 5:22-23

Lakini tunda ambalo Roho huzaa ni upendo, furaha, amani, subira, fadhili, wema, uaminifu, upole na kujitawala. Hakuna sheria inayopinga mambo kama haya.

04 Mithali 11:17

Watu wenye fadhili hujitendea mema, bali wakatili huiletea miili yao wenyewe madhara.

05 Luka 6:35

Badala yake, wapendeni maadui wenu, watendeeni mema, na mkopeshe bila kutarajia kurudishiwa chochote. Ndipo mtapata ujira mkubwa, nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu Kabisa, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasio na shukrani na kwa waovu.

06 Mithali 19:17

Anayemhurumia maskini anamkopesha BWANA, naye atamlipa kwa yale aliyoyatenda.

Mada zinazohusiana