Mistari ya Biblia Kuhusu Upendo katika Matendo

Mistari 12 ya Biblia kuhusu Upendo katika Matendo ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 1 Yohana 3:18

Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli.

02 Yakobo 2:15-16

Ikiwa ndugu yako au dada hana mavazi wala chakula, mmoja wenu akamwambia, “Enenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba,” pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini?

03 1 Yohana 3:17

Ikiwa mtu anavyo vitu vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu wakaaje ndani ya mtu huyo?

04 Wagalatia 5:13

Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo.

05 Mathayo 25:40

“Naye Mfalme atawajibu, ‘Amin nawaambia, kwa jinsi mlivyomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.’

06 Yakobo 2:17

Vivyo hivyo, imani peke yake kama haikuambatana na matendo, imekufa.

07 1 Yohana 4:11

Marafiki wapendwa, kama Mungu alivyotupenda sisi, imetupasa na sisi kupendana.

08 Wagalatia 6:10

Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio.

09 Waebrania 13:16

Na msiache kutenda mema na kushirikiana vile vitu mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mungu.

10 Warumi 12:9

Upendo lazima usiwe na unafiki. Chukieni lililo ovu, shikamaneni na lililo jema.

11 Luka 10:33-34

Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri alipomwona, alimhurumia. Akaenda alipokuwa na akasafisha majeraha yake kwa divai na mafuta, kisha akayafunga. Ndipo akampandisha kwenye punda wake, akampeleka mpaka kwenye nyumba ya wageni na kumtunza.

12 1 Wakorintho 13:3

Kama nikitoa mali yote niliyo nayo na kama nikijitolea mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu.

Mada zinazohusiana