Mistari ya Biblia Kuhusu Upendo Husitiri
Mistari 7 ya Biblia kuhusu Upendo Husitiri ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Jambo kuu kuliko yote, dumisheni upendo wenu ninyi kwa ninyi, uwe imara na usiokoma, kwa sababu upendo hufunika dhambi nyingi sana.
Chuki huanzisha ugomvi, bali upendo hutandika pazia juu ya kila kosa.
Hakuna jambo ambalo upendo hauwezi kulibeba, hakuna wakati unapoacha kuamini au kutumaini, hakuna jambo usiloweza kulistahimili.
Vumilianeni katika makosa yenu, na mtu akiwa na lalamiko dhidi ya mwenzake, msameheni. Bwana amewasamehe ninyi kwa ukarimu; nanyi lazima mfanye vivyo hivyo.
yule aliyefanya hivyo ajue jambo hili: mtu anayemrudisha mwenye dhambi kutoka katika njia yake potovu ataiokoa nafsi ya mwenye dhambi huyo kutoka mautini, na atafunika dhambi nyingi sana.
Anayesamehe kosa hujenga upendo, bali anayeendelea kulirudia huwatenganisha marafiki.
Kuweni wanyenyekevu na wapole kwa kila namna, na wavumilivu, mkichukuliana kwa upendo.