Mistari ya Biblia Kuhusu Ukarimu
Mistari 12 ya Biblia kuhusu Ukarimu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Kila mmoja wenu atoe kiasi alichoamua moyoni mwake, si kwa masikitiko, wala kwa sababu anajiona analazimika. Mungu anampenda mtu anayetoa kwa furaha.
Mtu mmoja hutoa kwa ukarimu na kupata zaidi; mwingine huzuia kinachopaswa kutolewa na kuishia katika uhitaji. Mtu mkarimu atafanikiwa, na anayewaburudisha wengine ataburudishwa.
Toeni, nanyi mtapewa: kipimo kilichojaa, kilichoshindiliwa, kilichotikiswa kikatulia, na kinachomwagika juu, kitamiminwa katika kunjo la vazi lenu. Kipimo mnachotumia kwa wengine ndicho kitakachotumiwa kwenu.”
Kumbukeni hili: mtu akipanda kidogo, atavuna kidogo; akipanda kwa wingi, atavuna kwa wingi.
Kwa kila njia nimewaonyesha mfano: kwa kufanya kazi kwa bidii hivi, ni lazima tuwasaidie walio dhaifu, na tuyakumbuke maneno ya Bwana Yesu, jinsi yeye mwenyewe alivyosema, ‘Kutoa kuna heri kubwa zaidi kuliko kupokea.’”
Watu wakarimu watabarikiwa, kwa sababu huwagawia maskini chakula chao.
Waambie watende mema, wawe matajiri katika matendo mema, watoe kwa ukarimu na kushirikiana na wengine.
Anayemhurumia maskini anamkopesha BWANA, naye atamlipa kwa yale aliyoyatenda.
Waponyeni wagonjwa, wafufueni waliokufa, watakaseni wenye ukoma, wafukuzeni pepo. Mlipokea bila kulipa, kwa hiyo toeni bila kudai malipo.
Tena msisahau kuwa wema na kugawana mlicho nacho ninyi kwa ninyi: Mungu hufurahia dhabihu za aina hiyo.
Yeyote anayewapa maskini hatakosa kitu, lakini yeyote anayegeuza macho yake mbali nao atapata laana nyingi.
Mambo huwaendea vema watu walio wema na kuwakopesha wengine, na wanaoshughulikia mambo yao kwa haki.