Mistari ya Biblia Kuhusu Kuwapenda Maadui
Mistari 5 ya Biblia kuhusu Kuwapenda Maadui ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
01 Mathayo 5:44
Lakini ninawaambia: Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi,
02 Luka 6:27-28
“Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya.
03 Warumi 12:20
Badala yake: “Kama adui yako ana njaa, mlishe; kama ana kiu, mpe kinywaji. Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.”
Kama adui yako ana njaa, mpe chakula ale; kama ana kiu, mpe maji anywe.
05 Warumi 12:14
Wabarikini wale wanaowatesa, barikini wala msilaani.