Mistari ya Biblia Kuhusu Faida ya Haki

Mistari 9 ya Biblia kuhusu Faida ya Haki ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mithali 13:11

Fedha isiyo ya halali hupungua, bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka.

02 Mithali 16:8

Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.

03 Mithali 20:23

Bwana anachukia sana mawe ya kupimia ya udanganyifu, nazo mizani zisizo halali hazimpendezi.

04 Walawi 19:35-36

“ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi. Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa halali, na hini halali. Mimi ndimi Bwana Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri.

05 Mithali 28:6

Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu.

06 Mithali 11:1

Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu, bali vipimo sahihi ni furaha yake.

07 Mithali 10:2

Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini.

08 Yeremia 17:11

Kama kware aanguaye mayai asiyoyataga, ndivyo alivyo mtu apataye mali kwa njia zisizo za haki. Maisha yake yafikapo katikati, siku zitamwacha, na mwishoni atabainika kuwa mpumbavu.

09 Walawi 19:13

“ ‘Usimdhulumu wala kumwibia jirani yako. “ ‘Usishikilie mshahara wa kibarua usiku kucha hadi asubuhi.

Mada zinazohusiana