Mistari ya Biblia Kuhusu Kuadibu kwa Upendo

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Kuadibu kwa Upendo ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mithali 13:24

Yeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe, bali yeye ampendaye huwa mwangalifu kumwadibisha.

02 Mithali 22:15

Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.

03 Waebrania 12:11

Kuadibishwa wakati wowote hakuonekani kuwa kitu cha kufurahisha bali chenye maumivu kinapotekelezwa. Lakini baadaye huzaa matunda ya haki na amani kwa wale waliofunzwa nayo.

04 Mithali 29:17

Mrudi mwanao, naye atakupa amani, atakufurahisha nafsi yako.

05 Mithali 3:11-12

Mwanangu, usiidharau adhabu ya Bwana na usichukie kukaripiwa naye, kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao, kama vile baba afanyavyo kwa mwana apendezwaye naye.

06 Mithali 19:18

Mrudi mwanao, kwa maana katika hiyo kuna tumaini, usiwe mshirika katika mauti yake.

07 Ufunuo 3:19

“Wale niwapendao, ninawakemea na kuwaadibisha. Hivyo uwe na bidii ukatubu.

Mada zinazohusiana