Mistari ya Biblia Kuhusu Kuchukuliana Mizigo

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Kuchukuliana Mizigo ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Wagalatia 6:2

Chukulianeni mizigo ninyi kwa ninyi, nanyi kwa njia hii mtatimiza sheria ya Kristo.

02 Warumi 15:1

Sisi tulio na nguvu, hatuna budi kuchukuliana na kushindwa kwa wale walio dhaifu wala si kujipendeza nafsi zetu wenyewe.

03 1 Wakorintho 12:26

Kama kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia pamoja nacho, kama kiungo kimoja kikipewa heshima, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.

04 Warumi 12:15

Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao.

05 Wakolosai 3:13

Vumilianeni na kusameheana mtu akiwa na lalamiko lolote dhidi ya mwenzake. Sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi.

06 Wagalatia 6:9-10

Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa. Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio.

Nasi twawasihi, ndugu, waonyeni walio wavivu, watieni moyo waoga, wasaidieni wanyonge na kuwavumilia watu wote.

Mada zinazohusiana