Mistari ya Biblia Kuhusu Kufanya Amani
Mistari 5 ya Biblia kuhusu Kufanya Amani ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
01 Mathayo 5:9
Heri walio wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.
02 Warumi 12:18
Kama ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote.
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao bila kuwa nao hakuna mtu atakayemwona Bwana.
Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani.
05 Yakobo 3:18
Mavuno ya haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.