Mistari ya Biblia Kuhusu Umoja
Mistari 14 ya Biblia kuhusu Umoja ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Wimbo wa kupanda. Wa Daudi. Ona uzuri wake na utamu wake, ndugu wanapoishi pamoja kwa maelewano!
Fanyeni kila juhudi kudumisha umoja ambao Roho huwapa, na amani iwe kifungo kinachowaunganisha.
basi ijazeni furaha yangu hadi ifurike: muwe na nia moja, mshikamane katika upendo uleule, muwe wamoja moyoni, na mwelekeze mawazo yenu kwenye lengo moja.
Baba, naomba wote wawe wamoja. Kama vile wewe ulivyo ndani yangu, nami nilivyo ndani yako, vivyo hivyo nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
Juu ya hayo yote vaeni upendo, ambao huunganisha kila kitu na kukifanya kikamilike.
Basi ndugu, nawasihi kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo: kubalianeni ninyi nyote, na pasiwe na migawanyiko kati yenu. Kile kilichochanika kishonwe upya, ili muungane pamoja, mkiwa na nia moja na kusudi moja.
Mungu, ambaye hutoa uvumilivu na faraja, awawezeshe kuishi kwa umoja kati yenu, kama Kristo Yesu apendavyo, ili kwa pamoja, kwa sauti moja, mumpe utukufu Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile kuna tumaini moja linalotokana na wito mlioupokea. Kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, Mungu mmoja, Baba wa wote, ambaye yuko juu ya wote, na kupitia wote, na ndani ya wote.
Kwa kweli, sisi sote tulibatizwa katika Roho mmoja tukawa mwili mmoja, tukiwa Wayahudi au Wagiriki, watumwa au watu huru, na sote tulipewa Roho mmoja tumnywe.
Muwe na mtazamo mmoja kati yenu. Msitamani mambo ya fahari, bali furahini kuandamana na watu wa hali ya chini. Msijione kuwa wenye hekima.
Kundi lote la waumini lilikuwa na moyo mmoja na nafsi moja. Hakuna hata mmoja wao aliyehesabu kitu chochote alichokuwa nacho kuwa chake peke yake; vyote walivyokuwa navyo vilikuwa mali ya wote.
Kwa ufupi: ninyi nyote mwe na umoja wa mawazo, mshiriki hisia za wenzenu, mpendane kama ndugu, mwe na mioyo ya huruma na mawazo ya unyenyekevu.
Jambo moja tu: ishini kama raia kwa namna inayostahili Injili ya Kristo. Hapo, nikija kuwaona au nikiwa mbali na kusikia habari zenu tu, nitajua kwamba mnasimama imara katika roho moja, mkishindana bega kwa bega kama mtu mmoja kwa ajili ya imani ya Injili,
Hatimaye, ndugu, furahini. Kubalini kurekebishwa, mfarijiwe, mwe na nia moja, na mdumishe amani kati yenu. Ndipo Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.