Mistari ya Biblia Kuhusu Urafiki

Mistari 13 ya Biblia kuhusu Urafiki ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mithali 17:17

Rafiki hupenda wakati wote naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.

02 Mithali 18:24

Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu, bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.

03 Yohana 15:13

Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

04 Mithali 27:9

Manukato na uvumba huleta furaha moyoni, nao uzuri wa rafiki huchipuka kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu.

05 Mhubiri 4:9-10

Wawili ni afadhali kuliko mmoja, kwa sababu wana malipo mazuri kwa kazi yao: Kama mmoja akianguka, mwenzake atamwinua. Lakini ni jambo la kuhuzunisha kwa mtu yule aangukaye naye hana wa kumwinua!

06 Mithali 27:6

Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu, bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.

07 Yohana 15:14-15

Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru. Siwaiti ninyi watumishi tena, kwa sababu watumishi hawajui bwana wao analofanya, bali nimewaita ninyi rafiki, kwa maana nimewajulisha mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu.

08 1 Samweli 18:1

Baada ya Daudi kumaliza kuongea na Sauli, roho ya Yonathani ikaambatana na roho ya Daudi, naye akampenda kama nafsi yake mwenyewe.

09 Mithali 13:20

Yeye atembeaye na mwenye hekima atapata hekima, bali rafiki wa mpumbavu hupata madhara.

10 Ayubu 6:14

“Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake, hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi.

11 Mithali 27:10

Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako, tena usiende nyumbani mwa ndugu yako wakati umepatwa na maafa. Bora jirani wa karibu kuliko ndugu aliye mbali.

12 Mithali 22:24-25

Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka, usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika, la sivyo utajifunza njia zake na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego.

13 1 Wakorintho 15:33

Msidanganyike: “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.”

Mada zinazohusiana